Wakaazi wa Dar walalama kuhusu usafiri TZ

Image caption Dala dala

Watu wengi hutumia mabasi madogo kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine mjini Dar Es Salaam nchini Tanzania.

Wakati wa muda wa kuelekea nyumbani watu hulazimika kupigania viti vichache vilivyopo huku wengine wakilzimika kutumia njia nyengine kuingia vyombo hivyo vya usafiri.

Image caption Usafiri Dar

Mabasi hayo yanayojulikana kama Dala Dala yalianza oparesheni zake miaka ya 70 ili kukabiliana na swala nyeti la ukosefu wa magari ya uchukuzi.

Wakati huo safari fupi iligharimu shilingi 5 za Tanzania ambazo zilikuwa sawa na dola moja na hivyobasi kuanza kwa jina la Dala Dala.

Image caption Uchukuzi Dar

Kwa sasa safari fupi hugharimu shilingi 500 za Tanzania ambapo ni robo ya dola moja.

Lakini bado abiria wanalalama kwamba wangetaka usafiri ambao ni rahisi na wenye kustarehesha.

Image caption Uchukuzi Dar Es Salaam

Wanasema kuwa hilo ni swala nyeti ambalo linafaa kupewa kipaumbele na serikali inayotarajiwa.

Madereva vilevile hulalamikia bei ya juu ya mafuta ya petroli pamoja na kodi za kiwango cha juu zinazotozwa na mamlaka.