Mtaalamu anadi haki za kuwapa nondo jina

Nondo Haki miliki ya picha Eric Metzler Ebay
Image caption Nondo hao waligunduliwa mara ya kwanza miaka minane iliyopita

Mtaalamu wa wadudu aliyegundua aina mpya ya nondo ameweka tangazo kwenye eBay akiuza haki za kuwapa nondo hao jina.

Eric H Metzler aligundua nondo hao New Mexico, Marekani miaka minane iliyopita, lakini ni majuzi tu ambapo walithibitishwa kuwa aina mpya ya nondo.

Kwa sasa, bei ya haki hizo mnadani imefikia $7,100 (£4,581) na zimesalia siku tatu kabla ya kufungwa kwa mnada huo.

Jina kutoka kwa atakayenunua haki hizo litahitaji kuandikwa kwa kilatini, na kuidhinishwa na wataalamu.

Pesa kutoka kwa mnada huo zitapewa Chama cha Mbuga za Kitaifa za Magharibi, kilichofadhili utafiti wa Bw Metzler.

"Mimi si tajiri na sina pesa nyingi za kutoa kusaidia jamii, lakini hii ndiyo njia pekee nilionelea ningetoa mchango wangu kwa binadamu,” amesema.