Kerry:Israeli na Palestina ziache uchochezi

Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewataka wapalestina na waisraeli kusitisha uchochezi

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewataka wapalestina na waisraeli kusitisha uchochezi uliosababisha vurugu zinazoendelea baina yao kwa haraka.

Waziri huyo amesema hayo akiwa mjini Berlin Ujerumani ambapo anashiriki mazungumzo na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hata hivyo Netanyahu amewalaumu wapalestina kuwa ndio walioanzilishi vurugu hizo.

Kerry amesema kuwa ni muhimu sana kutafuta mwafaka wa amani ya kudumu ilikuzuia maafa zaidi.

Kerry anatarajiwa kuweka wazi hali ilivyo kwenye maeneo ya kidini yanayohusishwa na vurugu hizo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kerry hayo akiwa mjini Berlin Ujerumani ambapo anashiriki mazungumzo na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Takriban watu 60 wameuwawa katika vurugu baina ya wapalestina na waisraeli kwa muda wa mwezi mmoja ulopita.

Hii leo asubuhi Kerry pamoja na Netanyahu wameshutumu mapigano hayo.

Hata hivyo Netanyahu amewalaumu wapalestina kuwa ndio walioanzilishi vurugu hizo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji wanaounga mkono Wapalestina wamekusanyika nje ya jengo la Chancellery ambapo Kerry anakutana na Netanyahu

Amemshtumu raisi wao Mahamoud Abbas kuwa ndiye anayesambaza uongo kuhusu hali ya maeneo ya kidini yanayohusishwa na machafuko hayo.

Ziara ya Netanyahu mjini Berlin tayari imekumbwa na wingu jeusi la utata.

Katika hotuba yake hapo jana, waziri huyo mkuu wa Israeli alisema kiongozi mpalestina ndiye aliyemshawishi aliyekuwa rais wa Ujerumani Adolf Hitler kutekeleza mauaji ya kimbari ya wayahudi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waisraeli kumi na wapalestina 47 wameuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita

Lakini baada ya mazungumzo na Netanyahu, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel alipuuzilia mbali matamshi hayo.

Kisa cha hivi punde zaidi katika wimbi hili ghasia,limetokea baada ya polisi wa Israeli kuwapiga risasi na kuwajeruhi wapalestina wawili ambao walimdunga kisu raia mmoja wa Israeli katika kituo cha Badu.

Waisraeli kumi na wapalestina 47 wameuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita katika makabiliano mabaya na visa vya kudungana visu.