Mama anayenusa ugonjwa wa kutetemeka 'Parkinson'

Image caption Mama anayenusa ugonjwa wa kutetemeka 'Parkinson'

Mama mmoja huko Scotland Uingereza amewaacha madaktari vinywa wazi kutokana na uwezo wake mkubwa na sahihi wa kunusa na kutambua watu walio na ugonjwa wa kutetemeka 'Parkinson'.

Uwezo wa kipekee wa mama huyo umewaacha wataalamu wamepigwa na butwaa kwani hakuna vipimo maalum vya kubaini nani ameambukizwa ugonjwa huo usio na tiba.

''Kwa sasa tunachokifanya ni kutazama mgonjwa na kuona ikiwa ana tetemeka na anashindwa kuzungumza na pia kama anakosa usingizi''Alisema daktari mkuu Dakta Tilo Kunath ambaye pia ni mhadhiri wa chuo cha Edinburg.

'Alichofanya bi Joy Milne ni cha ajabu na itasaidia sana kupunguza muda wa kubaini nani yuko katika hatari ya kuambukizwa na nani yuko salama.' Aliongezea Dakta Tilo Kunath

Image caption Bi Joy Milne na mumewe wakati wa maisha yake

Bi Joy Milne ni mjane kutoka Perth.

Mumewe aliaga dunia mwezi juni mwaka huu akiwa na umri wa miaka 65.

Kabla ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huu wa kukakamaa alikuwa ni mfanyikazi wa chumba cha upasuaji.

Aligunduliwa kuwa ameambukizwa ugonjwa huu miaka 20 iliyopita.

Joy anasema aligundua harufu fulani miaka 6 kabla ya mumewe kupatikana na ugonjwa huu.

Image caption Dakta Tilo Kunath ambaye pia ni mhadhiri wa chuo cha Edinburg.

''Harufu yake ilibadilika na kuwa kama ya tezi ya kulungu ama maski kwa mbali alianza kubadili harufu yake''

''Kwa kweli harufu ya mtu unayeishi naye kwa karibu utaijua tu'' alisema bibi huyo.

Lakini alipopatikana na ugonjwa huo ilimbidi mkewe aandamane naye kwenda kwenye mikutano ya shirika lisilokuwa la kiserikali la Parkinson UK huko ndiko alikogundua kila mtu alikuwa na harufu sawa na ile ya mumewe.

Kitivo cha bayologia cha chuo kikuu cha Edinburgh kiliposikia uwezo wake kiliwapa fulana watu 12; 6 walioambukizwa na 6 waliokuwa na afya nzuri.

Baada ya siku moja wakampa bi Joy fulana hizo na kwa mshangao Joy alipata sahihi harufu ya wagonjwa 6 waliokuwa.

Hata hivyo alisisitiza kuwa mmoja kati ya wale waliokuwa sawa alikuwa mwathiriwa wa ugonjwa huo wa kutetemeka na kulazimisha chuo hicho kufanya uchunguzi zaidi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ugonjwa huu umewaathiri watu wengi akiwemo bingwa wa masumbwi wa uzani wa juu Mohammed Ali

Tangu mwaka wa 1817 Dr James Parkinson alipogundua ugonjwa huo hakuna njia maalum ya kutambua.

Sasa chuo kikuu cha Edingburgh kinasema Joy amefungua mlango wa kupatikana njia maalum na moja kwa moja ya kubaini nani ana ugonjwa huo wa kukakamaa na nani hana.

Ugonjwa huu umewaathiri watu wengi akiwemo bingwa wa masumbwi wa uzani wa juu Mohammed Ali