Maandamano ya wanafunzi yachacha Afrika Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano ya wanafunzi yachacha Afrika Kusini

Wanafunzi nchini Afrika Kusini wametishia kufunga vyuo vikuu vyote nchini humo ili kupinga nyongeza ya karo.

Vyama vya wanafunzi vinapinga mpango wa serikali wa kupunguza mkopo wa karo ya chuo kwa wanafunzi maskini mwakani.

Aidha maafisa wa polisi walilazimika kufyatua risasi za plastiki na mabomu ya kutoa machozi ilikuwatanya wanafunzi waliokuwa wakiandamana katika miji mikuu ya Port Elizabeth na Durban.

Image caption Maafisa wa polisi wamekuwa na kibarua kigumu kuwazuia wanafunzi hao wasiingie katika majumba ya serikali

Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imetangaza kuwa itaongeza karo kwa asilimia 10% hadi 12%.

Waziri wa elimu aliwaahidi wanafunzi kuwa nyongeza hiyo haitapita asilimia 6% mwakani 2016 lakini hata hilo wanafunzi wamekataa.

Maandamano yanaendelea ya kupinga nyongeza hiyo ya karo.

Image caption Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika makabiliano hayo katika chuo kikuu cha Nelson Mandela Metropolitan mjini Port Elizabeth.

Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika makabiliano hayo katika chuo kikuu cha Nelson Mandela Metropolitan mjini Port Elizabeth.

Waandamanaji wanasema nyongeza ya karo itawafanya wanafunzi weusi kutoka familia maskini kukosa elimu kabisa.

Kufikia sasa vyuo vikuu 10 vimeathirika na makabiliano hayo baada ya muungano wa wanafunzi South African Students Congress (Sasco) kuitisha mgomo wa kitaifa.

Wanafunzi kadhaa wa chuo kikuu cha Cape Town (UCT) waliokamatwa watafikishwa mahakamani juma lijalo.

Image caption Kufikia sasa vyuo vikuu 10 vimeathirika na makabiliano hayo baina ya wanafunzi na maafisa wa usalama

Wanafunzi wanataka masomo ya chuo kikuu iwe ya bure kama ilivyoahidiwa na serikali ya ANC ilipochukua hatamu ya uongozi baada ya uhuru wa taifa hilo.

Waziri wa elimu Blade Nzimande amesema kuwa kwa sasa serikali hiyo haina uwezo wa kulipia wanafunzi wote karo ya shule.

Maandamano haya yaliaoanzia shuo kikuu cha Johannesburg Witwatersrand sasa yameenea hadi chuo kikuu cha Cape Town, Rhodes , Stellenbosch , Fort Hare , chuo kikuu cha Free State na Cape Peninsula University of Technology.

Aidha ripoti zinaashiria kuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Pretoria nao wameanza kuandamana.