Toyota; Magari milioni 6.5 yanahitilafu

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Magari milioni 6.5 yana hitilafu

Je una miliki gari aina ya Toyota, iliyoundwa kati ya mwaka wa 2005 na 2010 ?

Soma taarifa hii kwa makini.

Kampuni ya kutengenza magari ya Toyota imetoa ilani ya kurejeshwa magari zaidi ya milioni sita u nusu kote duniani.

Magari yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2005-2010 yamepatikana kuwa na hitilafu kwenye 'switch' mtambo wa kufunga na kufungua milango.

Yamkini Switch hiyo inakatika nyaya za kupitisha umeme na hivyo inaweza kusababisha gari kuwaka moto.

Magari yaliyopatikana na hitilafu hiyo ni aina ya Toyota Yaris, Toyota Corolla na Toyoto Camry.

Ilani hiyo ndiyo ya hivi punde zaidi kutokea katika kampuni hiyo ya Japan.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Magari yaliyopatikana na hitilafu hiyo ni aina ya Toyota Yaris, Toyota Corolla na Toyoto Camry.

Japo hakuna ajali yeyote iliyotokea kwa sababu ya hitilafu hiyo kuimarika kwa sheria zinazomiliki utengezaji wa magari umeifanya Toyota ichukue tahadhari kabla ajali.

Toyota iliagiza magari milioni 10 kote duniani kurejeshwa ili hitilafu ya mifuko ya hewa inayowakinga abiria na dereva wakati wa ajali.

Magari mengine yatakayo athirika ni Toyota RAV4 na Toyota Highlander miongoni mwa mengine.

Magari milioni 2.7 yaliuzwa Marekani magari 1.2 yako bara Ulaya na mengine 600,000 yako Japan kwa mujibu wa kumbukumbu za wanunuzi wa magari hayo.