Jinsi ya kupiga kura utakapofika kituoni

Kura
Image caption Baada ya kupiga kura, kidole chako kidogo mkono wa kushoto kitapakwa wino usiofutika kwa urahisi

Ufuatao ndio utaratibu wa kupiga kura:

1. Mkabidhi Msimamizi wa kituo kadi yako ya Kupigia Kura,

2. Jina lako litasomwa kwa sauti kubwa ili Mawakala wa Vyama vya Siasa waliopo kituoni wasikie,

3. Wasimamizi wa vituo, na hata Mawakala wa vyama vya siasa wakiwa na shaka wana haki ya kukuuliza maswali ili wajidhihirishe,

4. Msimamizi wa kituo atakukabidhi karatasi 3 za kura – yaani ya (Rais, Mbunge na Diwani) na pia atakuonyesha jinsi ya kukunja karatasi hizo,

5. Utaenda sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya Kupiga Kura yako,

6. Utaweka alama ‘✓’ ndani ya chumba kilichopo chini ya Mgombea unayemtaka.

7. Utatumbukiza karatasi zako za Kura katika masanduku ya Kura kwa jinsi utakavyoelekezwa.

8. Kabla ya kuondoka, utachovya kidole chako kidogo cha mkono wa kushoto katika wino maalum usiofutika kwa urahisi.

Chanzo: Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania