Filamu mpya ya Stars Wars yavunja rekodi

Star Wars Haki miliki ya picha DisneyLucasfilm
Image caption Filamu ya Star Wars: The Force Awakens itazinduliwa Desemba 17

Filamu mpya ya Star Wars: The Force Awakens imevunja rekodi Uingereza kwa kuuza tikezi nyingi zaidi siku ya kwanza ya kuuzwa kwa tiketi.

Tiketi hizo za mapema zilianza kuuzwa Jumanne, huku filamu hiyo ikitarajiwa kutolewa mara ya kwanza Desemba 17.

Saa 24 za kwanza, jumla ya tiketi 200,000 zilikuwa zimeuzwa, na kuvunja rekodi zilizokuwa zimewekwa awali na Skyfall, Spectre, The Hunger Games na Fifty Shades of Grey.

Nchini Marekani na Canada, Imax walifichua kwamba walipokea $6.5m (£4.2m) kutoka mauzo ya tiketi.

Pesa hizi ni nyingi mjo ukilinganisha na mauzo ya filamu za The Dark Knight Rises na Avengers: Age of Ultron siku ya kwanza, zote ambazo hazikupitisha $1m (£650,000).

"Tiketi zinanunuliwa sana kote, kuanzia Hollywood na London," alisema afisa mkuu mtendaji wa Imax Greg Foster.

Filamu ya The Force Awakens ndiyo ya saba katika msururu wa filamu za Star Wars na imeshirikisha waigizaji kama vile John Boyega, Daisy Ridley, Harrison Ford, Oscar Isaac na Adam Driver.