Watu sita wauawa msikitini Nigeria

Maiduguri
Image caption Mji wa Maiduguri umekuwa ukishuhudia mashambulio ya mara kwa mara

Watu sita wanahofiwa kufariki katika mji wa Maiduguri, Nigeria baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika msikiti mmoja mjini humo. Watu 12 wamejeruhiwa.

Maafisa wa huduma za dharura wanasema watano kati ya waliojeruhiwa wamo katika hali mahututi na wanapokea matibabu katika hospitali ya mafunzo ya Chuo Kikuu cha Maiduguri.

Baadhi ya wakazi wa Maiduguri, mji ulio kaskazini mashariki mwa Nigeria, wameeleza kutamaushwa kwao na ongezeko la mashambulio ya kujitoa mhanga eneo hilo, mwandishi wa BBC Bashir Sa'ad Abdullahi anasema.