Mahakama TZ:Sheria ya mita 200 iheshimiwe

Image caption Tume ya uchaguzi

Mahakama nchini Tanzania imesema kuwa hatoruhusu mtu yeyote kukaa umbali wa mita 200 kutoka kituo cha Kupigia Kura.

Image caption uchaguzi

Kulingana na taarifa iliotolewa na tume ya uchaguzi nchini humo na kutiwa sahihi na Mkurugenzi wa uchaguzi Kailima Ramadhan,mahakama hiyo vilevile imeamuru kwamba wapiga kura hawataruhusiwa kuvaa sare za Chama, kuonyesha nembo au upendeleo kwa mgombea yeyote au chama chochote wakati wa kupiga kura.

Image caption Tume ya uchaguzi

Taarifa hiyo inasema rasmi kuwa maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya vifungu vya maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, ambayo yanamzuia mtu yeyote kukaa umbali wa mita 200 bila sababu ya msingi katika vituo vya kupigia, kuhesabu na kujumlishia kura itaendelea kuheshimiwa.