Lubuva:Uchaguzi utafanyika bila matatizo

Image caption Mwenyekiti wa NEC Damian Lubuva

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania Jaji Damian Lubuva amesema kuwa ana matumaini kwamba uchaguzi utafanyika bila matatizo.

Image caption Vifaa vya kupigia kura

Vifaa vyote vya shughuli hiyo vimesafirishwa hadi katika vituo vya kupigia kura.

Image caption Vifaa vya kupigia kura

Anasema kwa kuwa kumekuwa na kampeni za amani, uchaguzi pia utafanyika bila tatizo lolote.

Image caption Vifaa vya kupigia kura

Awali BBC ilishuhudia jitihada za mara ya mwisho za wafanyikazi wa tume ya uchaguzi za kutuma vifaa katika maeneo ya kupigia kura kabla ya siku ya uchaguzi huo.