Wapenzi wafa maji wakiwa fungate

Image caption Maharusi walizama baharini wakati wakiwa katika fungate

Wapenzi kutoka Ireland kaskazini wamezama wakiwa katika fungate nchini Afrika kusini.

John na Lynette Rodgers kutoka walikutwa wamekufa katika ufukwe wa Plettenberg siku ya ijumaa.

Jitihada za kuokoa maisha yao ziligonga mwamba kwani walithibitishwa kufa katika eneo la tukio.

Kikosi cha uokoaji wamesema hali ya bahari ilikuwa mbaya wakati huo, kukiwa na mawimbi makali.

Inaaminika kuwa walikwenda kuogelea muda mfupi tu baada ya kutembelea eneo hilo maarufu kwa utalii.

Mtu mmoja alitoa kiashiria cha hali ya hatari baada ya kuona mwili wa Rodgers 28, kwenye ufukwe,Taasisi ya kitaifa ya uokoaji baharini imeeleza.

Wanawake wawili waliokuwa wakitembea pembezoni waliona mwili wa Lynette 26, takriban umbali wa mita 200.