Nchi za EU zafanya mkutano wa dharura

Haki miliki ya picha AP
Image caption wimbi la wahamiaji wanaoingia Ulaya wamesababisha hali ya mzozo miongoni mwa mataifa ya bara hilo

Viongozi wa nchi kadhaa za umoja wa Ulaya zinafanya mkutano wa dharura ili kuondoa tofauti zao kuhusu maswala ya wahamiaji.

Waziri Mkuu wa Slovenia Miro Cerar ameonya kuwa Umoja wa ulaya utaanza kusambaratika iwapo suala la wahamiaji halitatafutiwa ufumbuzi.

Lakini mwenzake wa Serbia, Aleksandar Vucic amesema hana uhakika kama watakuja na suluhu itakayosaidia kumaliza tatizo kwa haraka, lakini amesema ana uhakika nchini zinazohusika zitaweza kumaliza hali ya kulaumiana.

Nchi kumi za EU na mataifa ambayo sio wanachama wa EU wamekutana lakini kutokuwepo kwa Uturuki kwenye mazungumzo hayo kumezua maswali.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema mjadala utahusisha nchi ambazo zimekuwa zikikumbwa na wimbi la wakimbizi.