Debi ya Manchester yaisha sare tasa

Manchester City wanarejea kileleni mwa Ligi ya Premia baada ya kutoka sare tasa na Manchester United uwanjani Old Trafford.

City wana alama 22 sawa na Arsenal walio nambari mbili, lakini wamefunga magoli mengi.

Man United wako nambari nne na alama 20 sawa na West Ham ambao wamo nambari tatu kwa kuwa na tofauti kubwa ya mabao.

MECHI INAMALIZIKA Man Utd 0-0 Man City

Dakika 90+3 Mpira unakwisha. Manchester United 0-0 Manchester City

Dakika 90: Morgan Schneiderlin analishwa kadi ya njano kwa kumwangusha Kevin de Bruyne.

Dakika 87: Marouane Fellaini apiga mpira wa kichwa lakini hafanikiwi kufunga, Chris Smalling anajaribu tena lakini Hart anaudaka mpira.

Dakika 86: Aleksander Kolarov apiga frikiki safi, Nicolas Otamendi akaribia kufikia mpira huo lakini Wayne Rooney anamzima.

Dakika 84: Man Utd wakaribia sana kupata bao. Mpira wa mbali kutoka kwa Anthony Martial wamfikia Jesse Lingard anayekimbia mbio kulia, anamzidi Hart lakini mpira wake unagonga mwamba wa goli.

Dakika 80: Matteo Darmian aingia kucheza nafasi ya Antonio Valencia anayeonekana kuumia.

Dakika 76: Upande wa City Martin Demichelis anaingia nafasi ya Yaya Toure. Demichelis yamkini atakuwa na kibarua dhidi ya Fellaini.

Dakika 75: Anthony Martial ampiga chenga Bacary Sagna lakini anashindwa kwenda mbali na mpira.

Dakika 74: Marouane Fellaini aingia nafasi ya Bastian Schweinsteiger.

Dakika 69: Jesse Lingard anatoa pasi safi kwa Wayne Roone, lakini Rooney anashindwa kufikisha mpira kwa mchezaji wa Man Utd. Mambo bado Man Utd 0-0 Man City.

Dakika 65: Jesse Lingard aingia nafasi ya Juan Mata

Dakika 62: Juan Mata akwepa mtego wa kuotea aliowekewa na City. Anachomoka lakini Joe Hart anafanya mambo na kumzuia kufunga.

Dakika 57: Yaya Toure anapata mwanya na kujaribu kushambulia. Lakini Phil Jones anagundua ujanja wake na kumzima.

Dakika 53: Jesus Navas anaingia nafasi ya Sterling.

Dakika 53: Bastian Schweinsteigeranatoa pasi nzuri lakini Juan Mata hajamsoma vyema. Inapotea hivyo.

Dakika 50: Ander Herrera atoa kombora lakini linapinduliwa na kutoka nje. Inakuwa kona. Wakati wa kona, Herrera anaangushwa na Raheem Sterling. Man Utd wanataka penalti lakini wananyimwa.

Dakika 45: Kipindi cha pili chaanza.

MAPUMZIKO

Man Utd 0-0 Man City

Dakika 44: Vincent Kompany amwangusha Anthony Martial. Anapewa kadi ya njano.

Dakika 43:Wayne Rooney, afika nje tu ya eneo la hatari, anapokonywa mpira.

Mambo bado United 0-0 City

Dakika 40: Yaya Toure achapa frikiki. Inakosa lango.

Dakika 39: Juan Mata akabiliwa na kupokonywa mpira na Fernandinho, Mata ajibu kwa kumwangusha Mbrazil huyo kabla yake kufikisha mpira kwa Wilfried Bony. Mata analishwa kadi ya njano.

Dakika 37: Wayne Rooney anamponyoka Bacary Sagna, anajipenyeza ndani na kutoa pasi akidhamiria imfikie Anthony Martial, lakini wapi.

Dakika 32: Raheem Sterling apoteza mpira mzuri kutoka wingi ya kushoto.

Dakika 30: Kevin de Bruyne apiga frikiki lakini Bastian Schweinsteiger wa United aondoa mpira huo hatarini kwa kichwa.

Dakika 24: Rooney arejea uwanjani.

Dakika 22: Wayne Rooney atoka nje ya uwanja kupokea matibabu baada ya kugongana na Vincent Kompany.

Haki miliki ya picha Reuters

Dakika 17: Kevin de Bruyne aliyenunuliwa £50 ashambulia lakini hafanikiwi kupenya ngome ya United.

Dakika 13: Raheem Sterling ashambulia mara ya kwanza. Lakini azimwa na walinzi wa United.

Haki miliki ya picha Getty Images

Dakika 15: Anthony Martial apenya ndani kutoka wingi ya kushoto, na kukabili wachezaji wawili wa City. Mmoja wao Fernandinho amfyeka na kupewa kadi ya njano.

Dakika 9: Man Utd wataka wapewe penalti baada ya mpira kugusa mkono wa Fernandinho, mpira ukitoka kwa Juan Mata.

Dakika 6: Man Utd 0-0 Man City

City wanaonekana kuwa dhaifu sana kwenye winga huku Marcos Rojo akipitisha krosi. City hawajashambulia bado.

17:09 Antonio Valencia anamkabili Aleksandar Kolarov akitaka kupitisha krosi. Hajafanikiwa.

17:05 Man Utd 0-0 Man City

Mechi inaanza.

Kikosi cha United: Uwanjani: De Gea, Valencia, Jones, Smalling, Rojo, Schweinsteiger, Schneiderlin, Mata, Ander Herrera, Martial, Rooney. Benchi: Depay, Carrick, Blind, Romero, Fellaini, Lingard, Darmian.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Antony Martial amekuwa akitegemewa sana na Manchester City siku za karibuni

Kikosi cha City: Uwanjani: Hart, Sagna, Kompany, Otamendi, Kolarov, Fernando, Fernandinho, De Bruyne, Toure, Sterling, Bony. Benchi: Zabaleta, Caballero, Jesus Navas, Mangala, Demichelis, Roberts, Iheanacho.

Leo klabu mbili kutoka Manchester, Manchester United na Manchester City zinakutana uwanjani Old Trafford kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. Mechi itaamua ni nani atafunga siku ya leo akiwa kileleni kwenye jedwali la ligi.

Manchester City wanamkosa mfungaji wao matata Sergio Aguero lakini safu yao ya ulinzi imetiwa nguvu na kurejea kwa nahodha Vincent Kompany.

Meneja wa Manchester United Ijumaa alizua mjadala baada ya kusema City ndio walio katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda debi hiyo. Hata hivyo, alisema watajikakamua sana kushinda.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption De Bruyne na Sterling