Majibizano makali kuhusu wahamiaji Ulaya

Image caption Juncker amesema kuwa iwapo mataifa hayo hayatakubaliana haraka watu watapoteza maisha yao kwenye mito baridi ya Balkan

Kumeibuka majibizano makali baina ya viongozi wa mataifa ya bara ulaya katika mkutano wa kujadili hatima ya wahamiaji wanaoendelea kuingia Ulaya haswa wakati huu ambao msimu wa baridi kali unaanza.

Rais wa baraza la ulaya Jean-Claude Juncker, ameyataka mataifa ya Balkan yakome kuwaruhusu wahamiaji kuingia mataifa bila ilani.

Juncker amesema kuwa iwapo mataifa hayo hayatakubaliana haraka watu watapoteza maisha yao kwenye mito baridi ya Balkan kutokana na baridi kali inayoanza kushuhudiwa kusini mwa ulaya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri Mkuu wa Slovenia, Miro Cerar, ameonya kuwa Umoja wa Ulaya utaanza kusambaratika, iwapo hautochukua hatua za haraka na thabiti, ili kupambana na swala la wahamiaji

Katika mkutano huo Waziri Mkuu wa Slovenia, Miro Cerar, ameonya kuwa Umoja wa Ulaya utaanza kusambaratika, iwapo hautochukua hatua za haraka na thabiti, ili kupambana na swala la wahamiaji katika mataifa ya Balkan, yaani zile za Kusini Mashariki mwa Ulaya.

Bwana Cerar alisema hayo, kabla ya mkutano wa dharura, baina ya viongozi wa mataifa 10 ya Umoja wa Ulaya, na wenzao wa Albania, Serbia na Macedonia, mjini Brussels.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Majibizano makali kuhusu wahamiaji Ulaya

Wanatarajiwa kuzingatia mapendekezo kadha, pamoja na jinsi ya kutumia walinzi wa mpakani zaidi ya mia-nne, katika juma lijalo, kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi.

Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, alisema hali sasa inahitaji ufumbuzi nje ya mipaka ya Umoja wa Ulaya, ufumbuzi utao-i-ju-muisha Uturuki.