Rais mtarajiwa Tanzania kutangazwa Alhamisi

Image caption Kailima Kombo

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania kupitia mkurugenzi wake imesema kuwa inatarajia kwamba rais mtarajiwa atajulikana Alhamisi Oktoba 29 huku hafla ya kumpatia cheti cha kuchaguliwa ikifanyika tarehe 30.

Mkurugenzi huyo Kailima Kombo amesema kuwa watakuwa wakitoa matokeo ya uchaguzi huo kwa awamu kuanzia hapo kesho Jumatatu saa tatu asubuhi katika jumba la mikutano la Julius Nyerere.

Wakati huo huo afisa mmoja wa uchaguzi alionekana akiwapatia raia karatasi za kupigia kura ambazo tayari zalikuwa zimewekwa alama za upigaji kura.

Kulingana na Kailima, afisa huyo kutoka kituo cha kupigia kura mjini Dar es Salaam tayari amekamatwa.