Matokeo ya kura Tanzania kuanza kutangazwa Jumatatu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mpiga kura Tanzania

Kura zinahesabiwa katika uchaguzi mkuu wa Tanzania, ambapo wapigaji kura walijitokeza kwa wingi, kufuatana na taarifa ya Tume ya Uchaguzi.

Vituo vya kupigia vilifungwa jioni isipokuwa kwa wale ambao walikuwa vituoni, na bado hawakupiga kura.

Image caption Maelfu ya wapiga kura Tanzania

Mashindano yamekuwa makali kati ya wagombea wa chama tawala cha CCM, na umoja wa vyama vya upinzani.

Mgombea wa chama tawala, John Magufuli, alipambana na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye ali

Image caption Tume ya uchaguzi inasema matokeo ya kwanza yatatangazwa Kesho saa tatu asubuhi

kihama chama cha CCM na kuwa mwakilishi wa muungano wa vyama vya upinzani UKAWA.

Polisi wamewasifu watu kwa kupiga kura kwa salama, maneno ambayo pia yalikaririwa na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadan Kailima hapo awali.

Image caption Watanzania wakijivunia kuchangia mustakabali wa taifa lao

Na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, amesema matokeo ya uchaguzi wa rais yatatoka baada ya siku nne.