Argentina kuchagua mrithi wa Kirchner

Wapiga kura nchini Argentina wanachagua rais mpya kwenye uchaguzi mkuu utakaofikisha kikomo uongozi wa familia ya Kirchner wa miaka 12. Rais Cristina Fernandez de Kirchner ameongoza kwa mihula miwili mtawalia na, kwa mujibu wa katiba ya Argentina, hawezi kuwania tena. Mrithi wake alimeteua, Daniel Scioli ambaye anaegemea siasa za mrengo wa kushoto, anaongoza kwenye kura za maoni. Lakini anatarajiwa kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa  Mauricio Macri, meya wa Buenos Aires anayeegemea siasa za mrengo wa kati. Mgombea mwingine, Sergio Massa, mshirika wa zamani wa Kirchner, anamfuata Bw Macri kwa mujibu wa kura za maoni. Kuna wagombea wengine watatu wa urais. Uchaguzi huo wa Jumapili utakiwa wa awamu ya kwanza, na iwapo hakuna mgombea atakayepata asilimia 45 ya kura zote, au atakayepata zaidi ya asilimia 40 na awe mbele na asilimia 10 dhidi ya anayemfuata, basi kutakuwa na awamu ya pili Novemba 22. Atakayeshinda anakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi. Ingawa taifa hilo lilijikwamua kutoka kwa mgogoro wa kiuchumi 2002, uchumu wake umepunguza kasi ya ukuaji na mwaka jana ulikua kwa 0.5% pekee. Bi Kirchner alimrithi mumewe Nestor kama rais wa taifa hilo. Bw Nestor alifariki mwaka 2010, miaka mitatu baada yake kumkabidhi mkewe madaraka. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Kirchner ameongoza kwa mihula miwili inayoruhusiwa kikatiba

Wapiga kura nchini Argentina wanachagua rais mpya kwenye uchaguzi mkuu utakaofikisha kikomo uongozi wa familia ya Kirchner wa miaka 12.

Rais Cristina Fernandez de Kirchner ameongoza kwa mihula miwili mtawalia na, kwa mujibu wa katiba ya Argentina, hawezi kuwania tena.

Mrithi wake alimeteua, Daniel Scioli ambaye anaegemea siasa za mrengo wa kushoto, anaongoza kwenye kura za maoni.

Lakini anatarajiwa kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa

Mauricio Macri, meya wa Buenos Aires anayeegemea siasa za mrengo wa kati.

Mgombea mwingine, Sergio Massa, mshirika wa zamani wa Kirchner, anamfuata Bw Macri kwa mujibu wa kura za maoni. Kuna wagombea wengine watatu wa urais.

Uchaguzi huo wa Jumapili utakiwa wa awamu ya kwanza, na iwapo hakuna mgombea atakayepata asilimia 45 ya kura zote, au atakayepata zaidi ya asilimia 40 na awe mbele na asilimia 10 dhidi ya anayemfuata, basi kutakuwa na awamu ya pili Novemba 22.

Haki miliki ya picha AFP

Atakayeshinda anakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi.

Ingawa taifa hilo lilijikwamua kutoka kwa mgogoro wa kiuchumi 2002, uchumu wake umepunguza kasi ya ukuaji na mwaka jana ulikua kwa 0.5% pekee.

Bi Kirchner alimrithi mumewe Nestor kama rais wa taifa hilo. Bw Nestor alifariki mwaka 2010, miaka mitatu baada yake kumkabidhi mkewe madaraka.