Saa 'zakataa' kutii agizo la serikali Uturuki

Saa Haki miliki ya picha AP
Image caption Uturuki ilifaa kuongeza saa moja siku ya Jumapili

Raia nchini Uturuki walibaki kukanganyikiwa baada ya Serikali kuahirisha kurejeshwa nyuma kwa saa kama ilivyo kawaida kwa mataifa ya Ulaya.

Jambo lililokanganya watu ni kwamba baadhi ya saa huongozwa na kompyuta na hurejea nyuma bila kubadilishwa na mtu yeyote.

Saa hizi ‘hazikusikia’ agizo la serikali na zilibadilisha majira kama ilivyo kawaida.

Uturuki ilikuwa imepangiwa kurejesha saa nyuma baada ya kumalizika kwa siku Jumamosi Oktoba 24 pamoja na mataifa mengine. Hii ingefanya siku ya Jumapili kuwa na muda wa saa moja ya ziada. Lakini serikali Rais Recep Tayyip Erdogan iliamua wakati bora zaidi wa kutekeleza mabadiliko hayo ni baada ya uchaguzi.

Waturuki walitumia kitambulisha mada cha #saatkac - au "ni saa ngapi?" kutaniana kuhusu kunganganyikiwa kwa saa.

Uturuki, pamoja na nchi nyingine zilizo eneo la Saa za Ulaya Mashariki (EET) kama vile Bulgaria, Lithuania na Ukraine, na mataifa mengine, yalifaa kuongeza saa moja Jumapili.

Kwa mujibu wa viongozi Uturuki, kuchelewesha kurejesha nyuma saa kutawezesha wapiga kura kushiriki uchaguzi kukiwa bado mchana Novemba 1.

Baadaye, saa zitarejeshwa nyuma saa 04:00 mnamo Novemba 8.

Awali, kubadilisha saa kutoka saa za Afrika Mashariki hadi Ulaya mtu alihitaji kuongeza saa mbili lakini baada ya saa kurejeshwa nyuma, sasa watu wanaongeza saa tatu.