Mwanamke ‘wa ajabu’ kutoka India arejea nyumbani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Geeta ana matatizo ya kusikia na kuzungumza

Mwanamke kutoka India, aliyekwama Pakistan kwa mwongo mmoja bila kujulikana hasa alitoka eneo gani, amerejea nchini India.

Geeta aliwasili mjini Delhi Jumatatu asubuhi, baada yake kuweza kuwatambua watu wa familia yake kupitia picha zilizotumwa kutoka India.

Geeta, aliye na matatizo ya kuzungumza na kusikia, alikuwa na umri wa miaka 11 alipoingia kimakosa Pakistan.

Masaibu yalijulikana sana baada ya kutolewa kwa filamu ya Kihindi kwa jina Bajrangi Bhaijaan inayozungumzia kisa cha mwanamke Mpakistani ambaye hakuweza kuzungumza aliyekwama India.

Juhudi za kutafuta familia yake zilianza Agosti baada ya India kukubali kwamba ni raia wake.

Inaaminika aliweza kutambua familia moja kutoka jimbo la mashariki mwa India ya Bihar kuwa ndiyo familia yake. Jambo la kushangaza ni kwamba kuna familia nyingine mbili zinazodai yeye ni binti yao.

Kurejea nyumbani kwa Geeta kunaonekana kama kisa nadra ya ushirikiano wa utu kati ya mataifa hayo mawili hasimu.

"Hatutengani naye kabisa. Tutaendelea kuwasiliana naye,” Faisal Edhi, ambaye ni afisa wa shirika la kusaidia wasiojiweza lililomsaidia alipokuwa Pakistan amesema kwenye kikao na wanahabari, kabla ya Geeta kufunga safari kurejea India.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Geeta kwa sasa anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 22

Maafisa nchini India wanasema uchunguzi wa msambojeni (DNA) utafanywa kabla ya kumkabidhi kwa familia yoyote ile.

Iwapo familia yake halisi itakosekana, basi atatuzwa na kituo cha kuwatunza watu wasio na makao India hadi familia yake halisi ipatikane.

Geeta kwa sasa anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 22.