Ndege 11 zanaswa katika operesheni ya kumsaka Guzman

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ndege 11 zanaswa katika operesheni ya kumsaka Guzman

Waendesha mashtaka nchini Mexico, wametwaa ndege 11, silaha mbalimbali na mihadarati, wakati wa operesheni kali ya kumsaka mtoro mkuu wa mtandao wa dawa za kulevya Joaquin Guzman.

Ofisi ya mwanasheria mkuu nchini humo, inasema kwamba, wapelelezi wamevamia majumba kadha mali ya washukiwa katika majimbo matatu ikiwemo ile ya Sinaloa alikozaliwa Guzman.

Haki miliki ya picha AP
Image caption 'Shorty' - alitoroka gerezani mwezi Julai kupitia shimo iliyochimbwa chini kwa chini na kuibuka katika chumba chake gerezani.

Guzman, ambaye anafahamika sana kwa jina la utani El Chapo, au 'Shorty' - alitoroka gerezani mwezi Julai kupitia shimo iliyochimbwa chini kwa chini na kuibuka katika chumba chake gerezani.

Mapema mwezi huu maafisa wa usalama walidai kuwa bwana huyo mtoro alikuwa amekwepa mtego wa kikosi maalum cha kupambana na mihadarati japo alipata majeraha madogo mguuni.