UCHAGUZI 2015: YANAYOJIRI TANZANIA

MATUKIO MBALI MBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA YAKIWEMO MATOKEO YA UCHAGUZI

Bonyeza hapa kupata habari za karibuni zaidi

18.15:Cheza video

Huwezi kusikiliza tena

Hesabu ya kura imekuwa inaendelea na baadhi ya matokeo kutangazwa. Punde Tutaangalia matokeo yaliyotangazwa yanawaweka wapi wagombea wakuu, lakini kwanza huko Zanzibar ambayo ni ngome ya chama cha upinzani cha CUF kumekuwa na utata huku mgombea wa kiti cha Urais wa visiwa hivyo Maalim Seif akijitangaza mshindi hata kabla ya matokeo rasmi kutolewa na tume ya uchaguzi. Mwenzetu Sammy Awami amekuwa huko.

Image caption Viongozi wa UKAWA

15.07:Viongozi wakuu wa UKAWA wanaelekea Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza kesi na mashtaka ya wale vijana waliokamatwa juzi kwenye tallying centres za UKAWA. Vijana hao wamepelekwa mahakamani muda huu na inavyodaiwa tayari kuna hati ya kuzuia wasipate dhamana.

Image caption Waanzalizi nchini Tanzania

15.01: Waangalizi

Mkuu wa waangalizi wa muungano wa Ulaya katika uchaguzi mkuu wa Tanzania Judith Sargentini, amesema ukosefu wa jitihada pamoja na uwazi ndio sababu ya tume za uchaguzi za NEC na ZEC kukosa imani za vyama vyote vya kisiasa.

Amesema kwamba licha ya maandalizi mazuri kutoka tume hizo za uchaguzi, kutokuwepo kwa uwazi na ukosefu wa habari muhimu kuhusu sajili ya kupiga kura pamoja na mipaka katika majimbo mbali na mbinu inayotumiwa kutangaza matokeo ndio sababu zilizoathiri imani ya vyama hivyo kwa tume hizo za uchaguzi.

14.50:Cheza Video

Huwezi kusikiliza tena

Je,Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam una matokeo yapi.Mwanahabari wetu Robert Kiptoo anaripoti

Image caption Madaba,Ruvuma

14.43:Matokeo ya jimbo la Madaba mkoani Ruvuma

Image caption Jumba la matokeo ya uchaguzi kisiwani Zanzibar

14.34:Wanajeshi wamelizunguka jumba la matokeo ya uchaguzi kisiwani Zanzibar na kulifunga.Hakuna mtu anayeingia wala kutoka katika jumba hilo.

13.30:Cheza Video

Huwezi kusikiliza tena

Wakati matokeo yanazidi kumiminika mwandishi wetu Tulanana Bohela ametembelea mitaa ya Dar es es salaam na kutuletea taarifa ifuatayo.

Image caption CUF

12.40:Chama cha Upinzani kisiwani Zanzibar CUF kimetoa taarifa kikisema kinasikitishwa na mda unaochukuliwa na tume ya uchaguzi kisiwani humo kutoa matokeo.Kimesema kuwa hakioni sababu ya tume hiyo kutoa matokeo nusu nusu licha ya kuwa matokeo ya majimbo yote 54 yamehesabiwa kujumlishwa na kutolewa.

Image caption Matokeo yaendelea kutangazwa Zanzibar

12.19:Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar imesitisha utangazaji wa matokeo kwa muda baada ya umeme kukatika. Hata hivyo imeahidi kuendelea na matokeo hayo baada ya umeme kurudi muda mfupi baadaye.

Image caption Biashara zaanza kufunguliwa Dar Es Salaam

10.36: Biashara zimeanza kufunguliwa mjini Dar es Salaam nchini Tanzania huku wengi wa wawafanyibiashara wakiendelea kufunga biashara zao. Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara wanasema kuwa wataendelea kuzifunga hadi rais mpya atakapotangazwa.

Image caption Matokeo ya uchaguzi Zanzibar

11.03: Wanahabari wa vyombo vya ndani na nje ya nchi, pamoja na mawakala wa vyama vya siasa, wakiwa ndani ya ukumbi ambao Tume ya Uchaguzi Zanzibar inatangaza matokeo ya uchaguzi.

10.00: Mawaziri watano waangushwa

Mawaziri watano wa serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi katika majimbo yao,huku wagombea wengine wa Ubunge maarufu nao wakiangushwa na Kamba ya upinzani katika matokeo ya kura yanayoendelea kutolewa kufuatia uchaguzi mkuu nchini humo uliofanyika Jumapili.

Mawaziri hao watano wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete inayomaliza muda wake ni Stephen Wassira Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk Steven Kebwe Naibu Waziri wa Afya, Christopher Chiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayehusika na Uwekezaji na Uwezeshaji, Anne Kilango Malecela Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi na Omar Nundu aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Mawaziri hao walioangushwa katika majimbo yao wanaungana na wabunge wengine maarufu katika Bunge la Kumi la Tanzania waliong’ara ambao kwa sasa wameshindwa kurejea.

Hata hivyo pia wamo mawaziri wa Zamani Cyril Chami na Omary Nundu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania inaendelea kutangaza matokeo ya Ubunge na Urais.

Image caption Matokeo ya uchaguzi jimbo la Gando

09.00: Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Gando nchini Tanzania.

08.00: Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo.

Tayari tume ya uchaguzi imetoa matokeo ya majimbo 24 na bado inaendelea kutoa mengine zaidi. Huko Zanzibar, visiwa ambavyo kando na kutawaliwa na Rais wa Jamhuri, huwa pia na rais wake, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufikia sasa imetangaza matokeo ya majimbo 13 kati ya majimbo 54 yaliyoko visiwani humo.

Unaweza kupata habari zaidi kuhusu uchaguzi huo wa Tanzania uliofanyika Jumapili kwa kubonyeza hapa Tanzania: #uchaguzi2015.

ASUBUHI NJEMA