Wasiwasi watanda Zanzibar

Image caption Zanzibar

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeahidi kutoa matokeo zaidi ya uchaguzi mkuu kisiwani Zanzibar.

Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.

Vyombo vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza kuwa mshindi.

Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi yake.

Image caption Wasiwasi watanda Zanzibar

Mwandishi wetu, aliyeko huko anasema kuwa taharuki imetanda huko.

Maduka mengi yamesalia kuwa yamefungwa huku biashara ya kawaida na utalii ukiathirika.

Askari waliojihami wangali wamepiga doria mitaani

Zanzibar ina jumla ya wapiga kura 503,860 waliojiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Kwa habari zaidi kuhusu uchaguzi mkuu Tanzania boya kiunganishi hichi.