Waangalizi wataka matokeo kutolewa haraka TZ

Image caption Martina kabisana

Mkuu wa waangalizi wa muungano wa Ulaya katika uchaguzi mkuu wa Tanzania Judith Sargentini, amesema ukosefu wa jitihada pamoja na uwazi ndio sababu ya tume za uchaguzi za NEC na ZEC kukosa imani za vyama vyote vya kisiasa.

Amesema kwamba licha ya maandalizi mazuri kutoka tume hizo za uchaguzi, kutokuwepo kwa uwazi na ukosefu wa habari muhimu kuhusu sajili ya kupiga kura pamoja na mipaka katika majimbo, mbali na mbinu inayotumiwa kutangaza matokeo ndio sababu zilizoathiri imani ya vyama hivyo kwa tume hizo za uchaguzi.

Muungano huo uliwatuma waangalizi 141 ili kusimamia majimbo yote ya Tanzania siku ya uchaguzi.

Hatahivyo umeongezea kuwa vyombo vya habari vya kitaifa vilishindwa kuangazia kampeni kwa njia ya usawa.

Walivitaja vyombo vya habari vya serikali TBC na ZBC kwa kukipatia chama cha CCM mda mwingi huku vyombo vya habari vya kibinafsi vikiangazia kwa usawa.

Martina Kabisama naibu mwenyekiti wa muungano wa waangalizi wa uchaguzi Tanzania CEMOTCEMOT anaitaka tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC kutoa matokeo kwa haraka ili kuondoa wasiwasi.

Vilevile umetoa wito kwa maafisa wa polisi kuwaachilia vijana waliokamatwa iwapo hawana hatia.