NEC:Matukio Zanzibar hayataathiri Tanzania

Image caption 'Mchakato wa Uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utaendelea kama kawaida.''

Licha ya mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza kufutilia mbali kwa matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi,

Tume ya uchaguzi Tanzania NEC imetoa ilani kuwa hatua hiyo haitaathiri kwa njia yeyote matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania bara.

Kupitia kwa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa

Image caption Mgombea wa UKAWA Edward Lowasa alikuwa ameitaka NEC ifutilie mbali matokeo na ianze upya kuyahakiki

''Mchakato wa Uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utaendelea kama kawaida.''

''Uvumi unaoendelea kwamba, Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa umefutwa siyo kweli, ni uvumi, uongo, ni upotoshwaji.''

''Hadi sasa Tume imeshapokea matokeo ya kura za Rais kutoka majimbo yote ya Zanzibar na imeshayatangaza.''

Jaji Lubuva anaendelea kusema kuwa,

''Uchaguzi wa rais na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaosimamiwa na tume ya taifa ya uchaguzi ni tofauti na Uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.'

Image caption Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar (ZEC) Salim Jecha alifutilia mbali matokeo akisema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.

''Hii ni kwa sababu Tume hizi zinazisimamiwa na Katiba na sheria tofauti.'

''Uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano unasimamiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.''

Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar (ZEC) Salim Jecha alifutilia mbali matokeo akisema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.

Jecha aliwatuhumu baadhi ya makamishna wa tume yake kwa kuwa ''wawakilishi wa vyama vyao".

Image caption ''Uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano unasimamiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.''

" alikiri kuwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika."

Tangazo hilo limetokea wakati ambao taharuki imetanda kisiwani baada ya , mgombea wa chama cha upinzani cha Civic United From (CUF) Seif Sharif Hamad kujitangaza kuwa mshindi, hatua iliyokemewa na chama cha CCM ambacho mgombea wake Dkt Ali Mohamed Shein amekuwa rais wa visiwa hivyo muhula unaomalizika.

Tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa imetangaza matokeo yamajimbo 31 kati ya majimbo 54 visiwani humo.