Waziri wa ulinzi afutwa kazi CAR

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri wa ulinzi afutwa kazi CAR kufuatia mauaji kati ya wakristu na waislamu mwezi uliopita

Mawaziri wawili waliotuhumiwa kwa kuchochea mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 40 mwezi uliopita katika jamhuri ya Afrika ya Kati wamefutwa kazi.

Msemaji wa Afisi ya Rais ameiambia redio ya taifa kuwa aliyekuwa waziri wa ulinzi Marie-Noelle Koyara amesimamishwa kazi.

Nafasi yake sasa imechukuliwa na bwana Joseph Bidoumi ambaye amekuwa kiongozi wa kupigania haki za kibinadamu nchini humo.

Aidha msemaji huyo Clement Thierry Tito, aliiambia redio ya taifa kuwa aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani, Dominique Said Panguindji ameshushwa cheo.

Chrysostome Sambiandiye aliyeteuliwa kuwa waziri mpya wa usalama wa ndani ya taifa.

Mabadiliko hayo yametokea wakati ambao bunge la mpwito limemlaumu waziri mkuu Mahamat Kamoun kwa utepetevu wakati wa ghasia hizo za kidini zilizotibuka mjini Bangui mwishoni mwa mwezi Septemba.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu 40 waliripotiwa kufariki katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya kuuawa kwa dereva wa teksi.

Watu 40 waliripotiwa kufariki katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya kuuawa kwa dereva wa teksi.

Mamia ya watu walijeruhiwa kabla ya jeshi la kulinda amani la kimataifa kuingilia kati na kuwatawanisha wakristu na waislamu.

Bidoumi anamrithi bi Marie-Noelle Koyara,mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhfa huo katika historia ya taifa hilo.

Kwa upande wake Sambia anamrithi Dominique Said Panguindji, ambaye sasa atahudumu kama waziri wa haki mbali na kuwa msemaji wa serikali.

Uhasama wa kidini nchini humo ulianza mwaka wa 2013 baada ya kung'olewa madarakani kwa rais mkristu Francois Bozize, na makundi ya wapiganaji wa kiislamu wa Seleka.