UN yaonya jeshi la Machar Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption UN yaonya wafuasi wa Riek Machar Sudan Kusini

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kimeionya jeshi linalomuunga mkono kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar kuwa hatua yao ya kuteka mashua yake na maafisa wa kulinda amani ni makosa ya kivita.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa nchini humo bi Ariane Quentier ameithibitishia BBC kuwa waasi hao wamewaachia wanajeshi wa umoja wa mataifa waliokuwa wamewateka ila wamesalia na mashua yao.

Bi Quentier anasema kuwa wahudumu 12 wa kiraia waliokuwa kwenye mashua hiyo bado wameshikiliwa.

Msemaji huyo amewataka waasi hao kuwaachia huru mara moja.

Haki miliki ya picha
Image caption Msemaji huyo amewataka waasi hao kuwaachia huru mara moja.

Aidha ameonya kuwa waasi hao wamewaibia mafuta silaha na vifaa vyengine vya thamani.

Hata hivyo msemaji wa waasi hao (James Gatdet Dak) amesema kuwa tukio hilo halikuwa limekusudiwa kwani anasema kuwa walinda usalama hao wa umoja wa mataifa hawakutoa ilani yao kutumikia mtumbwi huo kwenye mto Nile.

Aidha bwana Dak amewataka wanajeshi hao wa kulinda amani kuwa na ushirikiano wa karibu nao ilikuepuka matukio mengine kama hayo.