Uingereza yapinga kufutwa matokeo Zanzibar

Image caption Uingereza

Serikali ya Uingereza na ile ya Ireland Kaskazini zimepinga kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.

Serikali hizo zimesema kuwa hazioni sababu ya kufutwa kwa matokeo hayo baada ya waangalizi wa kimataifa kufurahishwa na vile uchaguzi huo ulivyofanyika kwa amani.

Mataifa hayo sasa yanaitaka tume ya Uchaguzi kisiwani humo ZEC,kuorodhesha matokeo hayo mara moja bila kuchelewa.

Mataifa hayo vilevile yamewapongeza raia wa Tanzania kwa kufanya uchaguzi wa amani huku wakiwataka wanasiasa husika kutafuta suluhu ambayo itaambatana na matakwa ya raia wa Zanzibar kama walivyopitisha katika chaguzi huo wa tarehe 25.