Gesi kutoka Israeli yaua mtoto Mpalestina

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mabomu ya gesi ya Israeli yaua mtoto wa miezi 8 mpalestina

Wizara ya afya ya Palestina imethibitisha kuwa mtoto wa miezi 8 amefariki dunia baada ya kupumua gesi kali iliyotupwa na majeshi ya Israeli dhidi ya vijana waliokuwa wakiandamana huko Bethlehem.

Moshi wa bomu hilo la kutoa machozi ulienea hadi nyumbani kwa mtoto huyo huko Bethlehem.

Msemaji wa jeshi la Israeli amesema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Msemaji wa jeshi la Israeli amesema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kifo cha mtoto huyo wa miezi minane tu Ramadan Thawabteh , kimeongeza idadi ya wapalestina waliouawa hadi kufikia sasa kuzidi 60 katika kipindi cha mwezi mmoja.

Inakisiwa kuwa takriban waisraeli 9 wameuawa na wapalestina katika kipindi hicho.