UN yawafutwa kazi 5 kwa utovu wa nidhamu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption UN yawafutwa kazi 5 kwa utovu wa nidhamu

Wafanyikazi 4 wa Umoja wa Mataifa wamefutwa kazi baada ya kutizama filamu ya ngono kwenye mtandao wa intaneti wa shirika hilo la kimataifa.

Kibarua cha mfanyikazi mwengine kiliota nyasi baada ya kupatikana na kosa la kusafirisha kilo 173 ya bangi katika gari la kazi.

Visa hivyo vyote vilifanyika kati ya Julai mosi mwaka uliopita na juni tarehe 30 mwaka huu.

Hata hivyo ripoti hiyo ya UN haijabainisha iwapo walifunguliwa mashtaka au la.

Ripoti hiyo hutolewa na shirika hilo kwa lengo la kutoa tathmini ya wafanyikazi wake 41,000 na kuonesha hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao.

Hata hivyo taarifa hiyo haisemi walikokuwa wanafanya kazi na tarehe kamili waliofutwa kazi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msemaji wa UN, Farhan Haq, aliiambia BBC kuwa kesi zote dhidi ya wafanyikazi wa umoja wa mataifa hushughulikiwa na afisi moja tu.

Msemaji wa UN, Farhan Haq, aliiambia BBC kuwa kesi zote dhidi ya wafanyikazi wa umoja wa mataifa hushughulikiwa na afisi moja tu.

Mfanyikazi mwengine alifutwa kazi baada ya kuiba dola 2,200 kutoka kwenye mkoba wa abiria.

Alikuwa analinda uwanja wa ndege uliokuwa unasimamiwa na shirika hilo.

Mwengine alibeba abiria kwenye gari la UN bila idhini huku mwengine akifukuzwa kazi baada ya kuwaruhusu waandishi wa habari kuingia katika eneo wasiloruhusiwa.