Yamaha kuunda roboti ya kuendesha pikipiki

Roboti
Image caption Roboti hiyo itaweza kufanya uamuzi kuhusu njia ya kufuata

Kampuni ya Yamaha Motors imefichua kwamba inaunda roboti ambayo itaweza kuendesha pikipiki ambazo hutumiwa kwenye mashindano ya pikipiki.

Kampuni hiyo kutoka Japan ilionyesha mfano wa roboti hiyo katika maonyesho ya magari na pikipiki ya Tokyo Motor Show.

Ingawa kwa sasa roboti hiyo inategemea kuongozwa na mtu, roboti kamili itakayozinduliwa mwishowe itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu njia bora zaidi ya kufuata na kufikia kasi ya juu zaidi ikizunguka uwanja.