Wachunguzi wa Urusi wawasili Misri

Image caption Wachunguzi wa Urusi wawasili Misri

Mawaziri wa Urusi wanaohusika na usafiri na ajali, wamewasili kwenye eneo nchini Misri ambako ndege ya Urusi ilianguka hapo jana.

Hadi sasa inaaminika kuwa hakuna abiria yeyote aliyenusurika kati ya 224.

Mawaziri hao wamefuatana na mkuu wa idara ya safari za ndege ya Urusi, kuwasaidia maafisa wa Misri, wanaojaribu kutafuta chanzo cha ajali hiyo.

Hadi sasa, miili 175 ndio imepatikana.

Pamoja nao wachunguzi wa Urusi wamewasili nchini humo kupiga msasa sababu zilizosababisha kilisabasisha kuanguka kwa ndege hiyo ya Urusi katika rasi ya Sinai .

Maaafisa nchini Misri na Urusi wamekana madai kutoka kwa kundi la Islamic State kuwa ndilo liliangusha ndege hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mahala ilikoanguka ndege ya Urusi

Waziri mkuu nchini Misri Sherif Ismail alisema kuwa tatizo la kiufundi huenda ndilo lilisabaisha kuanguka kwa ndege hiyo.

Vinasa sauti vyote vye ndege hiyo vimepatikana na vitakaguliwa na wachungzui wa Urusi.

Licha ya matamshi hayo mashirika ya ndege ya Emirates, Air France na Lufthansa yamesitisha safari zao katika anga ya Sinai hadi pale habari zaidi zitakapotolewa.