Korea, China na Japan zakutana

Image caption Korea, China na Japan zakutana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 3

Viongozi wa Korea Kusini , China na Japan wanafanya mazunguzo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka mitatu.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na waziri mkuu wa China Li Keqiang wamesafiri kwenda mji mkuu wa Korea Kusini Seoul kukutana na rais wa nchi hiyo Park Geun-hye.

Mikutano kati ya viongozi hao ilisitishwa mwaka 2012 kutokana na mivutano ya mipaka na vitendo vya Japan wakati wa vita vya pili vya dunia.

Uchina na Korea zinahisi kuwa Japan haijaonesha kujutia matendo yake haswa wakati wa vita vya pili vya dunia.

Wadadisi wanahisi kuwa mataifa hayo matatu yangali na ati ati kuhusiana na swala la mipaka.

Hata hivyo Lengo la mkutano huo ni kurejesha uhusiano na kuongeza ushirikiano ya biashara kati yao.