FBI yakanusha mashua ya rais wa Maldives ilitegwa bomu

Haki miliki ya picha FBI
Image caption FBI haijapata ushahidi wa kuthibitisha kuwa mlipuko uliotokea kwenye mashua ya rais wa Maldives Abdullah Yameen, mwezi Septemba ulisababishwa na bomu

Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI linasema kuwa halijapata ushahidi wa mwisho kuweza kuthibitisha kuwa mlipuko uliotokea kwenye mashua iliyokuwa imembeba rais wa visiwa vya Maldives Abdullah Yameen, mwezi Septemba ulisababishwa na bomu lililotegwa humo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption FBI yapinga mashua ya rais wa Maldives ilitegwa bomu

Makamu wa rais Ahmed Adheeb alikamatwa wiki iliyopita kwa kuhusika katika njama hiyo.

Japo rais yameen hakujeruhiwa mkewe na maafisa wengine wawili walijeruhiwa katika mlipuko huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makamu wa rais Ahmed Adheeb alikamatwa wiki iliyopita kwa kuhusika katika njama hiyo

Taarifa ya FBI ambayo ilitolewa na gazeti la Wall Street inaonekana kukinzana na ile ya wachunguzi wengine wa kimataifa ambao serikali ya Maldives inasema walibaini kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu.

Taifa hilo la bahari hindi limekuwa na mvutano wa kisiasa katika miaka ya hivi karibuni.