Wafyatuliana risasi katika uchaguzi Pakistan

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapinzani wafyatuliana risasi katika uchaguzi Pakistan

Wanajeshi wametumwa kusini mwa Pakistan kutuliza hali baada ya watu 11 kuuawa wakati wa mapigano kati ya mahasimu wa kisiasa.

Takriban watu wengine 35 walijeruhiwa.

Maafisa walisema kuwa wafuasi wa vyama hasimu vya kisiasa walifyatuliana risasi katika mkoa wa Sindh katika mji wa Ranipur ulioko Khairpur.

Duru hata hivyo zinasema kuwa makabiliano yalitibuka baiana ya wafuasi wa Pakistan Peoples Party (PPP) na Pakistan Muslim League-Functional(PML-F).

Uchunguzi umeanza ilikubaini kiini haswa cha makabiliano hayo.

Haki miliki ya picha afp
Image caption Takriban watu wengine 35 walijeruhiwa.

Ghasia hizo zilianza wakati wapiga kura waliingia katika vituo vya kupigia kura kwenye uchaguzi wa kieneo.

Upigaji kura katika mji huo uliahirishwa mara moja.

Majimbo ya Punjab na Sindh yanaandaa uchaguzi wao leo.