Shambulizi laua 15 mjini Mogadishu

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Somalia inasema kuwa takriban watu 15 wameuwa

Utawala nchini Somalia unasema kuwa takriban watu 15wameuwa wakati wanamgambo waliposhambulia hoteli moja mjini Mogadishu.

Hoteli hiyo ambayo iko kwenye moja ya mitaa yenye shughuli nyingi mjini humo mara nyingi hutumiwa na wabunge na maafisa wa serikali.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shambulizi laua 8 mjini Mogadishu

Kundi la kiislamu la al Shabaab lilisema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo.

Vikosi vya muungano wa Afrika vinasema kuwa vimechukua udhibiti wa hoteli hiyo baada ya mapigano makali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption al shaabab wanasema ndio waliendesha shambulizi

Ripoti zinasema kuwa mlipuko huo ulifuatiwa na ufyatulianaji mkubwa wa risasi.