Mashambulizi ya angani yawaua 60 Allepo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashambulizi ya angani yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 60

Wanaharakati wanasema kuwa zaidi ya watu 60 wameuawa na jeshi la Syria katika mashambulizi ya angani yanayoendeshwa na Urusi katika mkoa wa kaskazini wa Aleppo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Shirika la kupigania haki za binadamu lenye makao yake Makuu nchini Uingezea, lilisema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika katika mji wa Aleppo na miji mingine kadha na hata vijijini.

Image caption Marekani na Urusi zimekubaliana kuzindua mchakato mpya wa amani Syria

Siku ya Ijumaa zaidi ya watu 70 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya angani kwenye soko moja katika eneo lonalodhibitiwa na waasi la Douma.

Kuongezeka kwa ghasia kunajiri wakati nchi kadha zikiwemo Marekani na Urusi kukubaliana wakati wa mazungumzo mjini Vienna siku ya ijumaa, kuzindua mchakato mpya wa amani kati ya serikali ya Syria na makundi ya waasi.