Iran yaanza kutekeleza mkataba wa nyuklia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtambo wa nyuklia wa Arak

Iran imeanza kutekeleza vipengee vya mkataba wa kufuta mradi wake wa nyuklia iliyokubaliana na mataifa ya makubwa duniani.

Afisa mkuu wa nishati ya nyuklia nchini Iran, anasema kuwa taifa hilo limeanza kupunguza urutubishaji wa nuklia, kuambatana na makubaliano hayo.

Ali Akbar Salehi, amesema kwamba kazi imeanza, lakini utekelezaji kamili utachukua muda kidogo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iran ilikubaliana mwezi Julai kudhibiti shughuli zake za kinyuklia

Runinga ya taifa la Iran, imesema kuwa, wabunge 20 wenye misimamo mikali wamemuandikia barua rais wa nchi hiyo kulalamika kuwa taratibu ya kuharibu mitambo hiyo ya kinyuklia inafanyika haraka kuliko inavyotarajiwa

Iran ilikubaliana mwezi Julai kudhibiti shughuli zake za kinyuklia, ili iondolewe vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa.