Utata chanzo cha ajali ya ndege Misri

Haki miliki ya picha epa
Image caption Mabaki ya ndege iliyopata ajali

Utata umeendelea kugubika ajali ya ndege iiyodondoka katika katika rasi ya Sinai huko nchini Misri na kuua abiria wote mia mbili na ishirini na nne walikufa.

Wakati mkuu wa Mamlaka ya Anga ya nchini Urusi akisema ni mapema mno kutabiri chanzo cha ajali hiyo, wamiliki wa ndege hiyo wamesema ajali hiyo imesababishwa na nguvu kutoka nje.

Ni wazi sasa kila mtu amekuwa akizungumza cha kwake kuhusu ajali hiyo aliyopoteza maisha ya watu zaidi ya mia mbili wengi wao wakiwa ni raia wa Urusi ambapo wakati mkuu wa mamlaka ya anga nchini Urusi Aleksandar Neradko akisema ni mapema mno kukisia chanzo cha ajali hiyo wapo wanaona huenda ni makosa ya rubani au tatizo la kiufundi ambalo limesababishwa na nguvu kutoka nje.

Ndege hyo Metrojet ilivunjika vipande ikiwa angani na kuua abiria wote waliokuwemo ndani yake.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndugu ya waliopata ajali wakifarijiana

Balozi wa Urusi nchini Misri Serge Kirpichenko anasema itachukua muda kabla ya kupata taarifa sahihi kutoka kisanduku cheusi kilichorekodi tukio hilo.

"Uchunguzi kwenye kisanduku cheusi tayari umeshaanza lakini ni katika hatua za awali katika siku ya kwanza ya uchunguzi. Uchunguzi unaweza kuchukua wiki kadhaa, siku siku kadhaa kwa sababu ni kazi nguvu na yenye changamoto kubwa na kwa hiyo hakuna mtu anayeweza kufikia hitimisho mapema. Ni lazima tuwe na uhakika kila taarifa ni sahihi na sidhani kuna haja ya kupotosha kuhusu chanzo cha ajali hii."

Naye Mkuu wa Idara ya Upelelezi nchini Marekani James Clapper amesema ni mapema mno kusema ndege hiyo ilitunguliwa na wanamgambo wa Islamic State.

"Hatuna ushahidi wa moja kwa moja kuonyesha kuwa ni tukio la kigaidi. ISIL wame tweet wakisema wanahusika na ajali hiyo na tunajua wanamgambo hao wana nguvu katika eneo hilo la Sinai, lakini hatujui kama ni kweli mimi ninafikiri mara kisanduku cheusi kitakapochunguzwa ambacho tayari kimeshapatikana labda tutaelewa zaidi ukweli. Je ISIS wana uwezo wa kutungua ndege Inawezekana lakini hatuwezi kuthibitisha moja kwa moja."