Je, mitandao husababisha magonjwa ya zinaa?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapendanao wanaokutanishwa na mitandao

Mitandao ya kuwakutanisha wapendanao inaongeza viwango vya magonjwa ya zinaa, kulingana na muungano wa wanaosimamia afya ya ngono na maambukizi ya ukimwi nchini Uingereza.

Mmoja wa madaktari bingwa anayeongoza katika afya ya ngono nchini Uingereza, amesema kwamba mitandao hiyo inapaswa kuwekeza katika muda zaidi ili kushinikiza ujumbe wa ngono salama.

"Unaweza kuwabadilisha mara kwa mara wapenzi kwa kutumia mtandao, na kila unavyowabadilisha kwa haraka, tishio la kuambukizwa linaongezeka", Dr Peter Greenhouse ameambia Newsbeat.

Kitu kinachonitia wasi wasi ni kwamba tunakalibiwa na tishio kubwa la maambukizi ya HIV.

Image caption Wapendanao waliokutanishwa na mitandao

Wamiliki wa mitandao ya kuwakutanisha wapendanao wanasema kwamba mitandao hio inakuza ngono salama, huku wengine wakidai kuna viwango vya chini vya wanaoambukizwa.

Lakini Dr Greenhouse amesema kwamba mitandao hiyo inaweza kuwa tishio kubwa kwa afya ya wanaoitumia kingono.

"Iwapo idadi fulani ya watu wanabadilisha wapenzi haraka, bila kujali huenda wameambukizwa, husababisha mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya ukimwi. Mitandao hiyo inaweza kusababisha hilo".

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mitandao inaowakutanisha wapendanao

Kituo kimoja nchini Uingereza kinachosimamia afya ya ngono, na ambacho kinaendesha 'mtandao wa kusaidia kliniki, kinasema kwamba kinawasaidia mara kwa mara makumi ya wagonjwa kila mwezi.

Takwimu za hivi karibuni kutoka idara ya afya ya uma nchini Uingereza, zinaonyesha ongezeko la magonjwa ya zinaa.