Dereva wa teksi ya Uber afungwa maisha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shiv Kumar Yadav,alipatikana na makosa matatu ikiwemo kubaka mteja wake

Dereva wa teksi wa kampuni inayotoa huduma ya pamoja ya teksi- Uber, amehukumiwa jela maisha nchini India kwa kumbaka mwanamke mmoja abiria wake mwezi Disemba mwaka jana.

Mahakama maalum inayotoa hukumu zake moja kwa moja mjini Delhi imempata na hatia, dereva Shiv Kumar Yadav, na makosa matatu aliyokuwa akikabiliana nayo ikiwemo kubaka, na kumteka nyara mwanamke wa miaka 26.

Mwanamke huyo anasema kuwa kisa hicho kilifanyika katika sehemu ya siri, baada ya yeye kusinzia akiwa ndani ya Texi.

Kampuni ya Uber, baadaye ilizuiwa kuendeshahuduma hiyo katika mji mkuu wa India.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Kampuni hiyo ililaumiwa kwa kutowapiga msasa madereva wake.

Kampuni hiyo ililaumiwa kwa kutowapiga msasa madereva wake.

Lakini bado inafanya kazi katika baadhi ya miji mingine nchini india.