Aliyekuwa rais wa IAAF afunguliwa mashtaka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa rais wa IAAF afunguliwa mashtaka

Ufaransa imeanzisha uchunguzi dhidi ya aliyekuwa rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF,Lamine Diack, kuhusiana na madai ya ufisadi .

Viongozi wa mashtaka nchini humo wanadai kuwa huenda raia huyo wa Senegal alipokea hongo kwa nia ya kuzuia kupigwa marufuku kwa wanariadha waliopatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Diack anadaiwa kuahirisha marufuku ya wanariadha kutoka Urusi waliopatikana na hatia mwaka wa 2011.

Diack anadaiwa kuahirisha marufuku ya wanariadha kutoka Urusi waliopatikana na hatia mwaka wa 2011.

Diack alistaafu baada ya kuongoza shirikisho hilo la riadha IAAF kwa kipindi cha miaka 16

Diack na mshauri wake Habib Cisse walikamatwa siku ya jumapili na kuachiliwa huru jumanne baada ya kuhojiwa na polisi na majaji.

Haki miliki ya picha AP
Image caption IAAF imelaumiwa kwa kupuuza ripoti za matumizi ya madawa miongoni mwa wanariadha.

IAAF imeahidi kushirikiana na maafisa wanaochunguza madai hayo.

Tayari wapelelezi wamefika katika makao makuu ya IAAF huko Monaco kufanya upepelezi na mahojiano na maafisa husika.

Majuzi shirikisho hilo la riadha IAAF lilishtumiwa kwa kukandamiza ripoti iliyofichua kuwa thuluthi moja ya wanariadha nyota walikuwa wanatumia madawa ya kututumua misuli yaliyopigwa maraufuku.

IAAF imelaumiwa kwa kupuuza ripoti za matumizi ya madawa miongoni mwa wanariadha.