Suu Kyi aahidi kuwa juu ya rais Myanmar

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suu Kyi ahidi kuwa juu ya rais Myanmar

Kiongozi wa upinzani nchini Myanmar Aung San Suu Kyi ameahidi wafuasi wake kuwa ataongoza serikali ikiwa chama chake cha National League for Democracy kitashinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Chini ya katiba iliyoundwa na jeshi haruhusiwi kugombea urais.

Huo ndio uchaguzi wa kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka 25.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suu Kyi alisema kuwa iwapo chama chake kitashinda uchaguzi mkuu huu, basi atamchagua rais ambaye ataongoza kwa mujibu wa kanuni za chama chake cha National League for Democracy

Lakini akihutubia mkutano wake wa mwisho wa hadhara katika mji mkubwa zaidi nchini humo Yangon,Suu Kyi alisema kuwa iwapo chama chake kitashinda uchaguzi mkuu huu, basi atamchagua rais ambaye ataongoza kwa mujibu wa kanuni za chama chake cha National League for Democracy.

Mwandishi wa BBC aliyeko Myanmar anesema kuwa tamko hilo litachukuliwa kama ushindani wa moja kwa moja hdidi ya jeshi la taifa hilo na huenda ikasemekana kuwa anakwenda kinyume cha katiba.