Ben Carson:Wanahabari wananiharibia jina

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ben Carson kushoto

Mmoja wa wagombeaji wa Urais nchini Marekani, aliye mstari wa mbele katika chama cha Republican, Daktari bingwa wa upasuaji aliyestaafu, Ben Carson, ameshutumu vyombo vya habari kwa kile alichosema ni nia yao ya kumchafulia jina.

Tamko lake linatokana na maswali aliyoulizwa kuhusiana na kitabu juu ya maisha yake alichochapisha miaka ya 90 ambapo inasemekana alipewa karo kwenda kusoma katika Shule maalumu ya kijeshi ya West Point.

Alisema kuwa hakuomba msaada huo wa karo na wala hakupewa nafasi hiyo na kwamba ripoti zinazochapishwa hivi sasa zinatokana na mazungumzo aliyoyafanya na baadhi ya maafisa wa vyeo vya juu Serikalini.

Mpinzani wake mkuu katika chama cha republican alichapisha habari katika mtandao wa kijamii wa Twitter akisema: "Wau, hiyo ni sehemu ndogo tu ya uongo anaotulimbikizia Ben Carson."