Ronaldo asema ndiye bora zaidi duniani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Cristiano Ronaldo

Mimi ndiye mchezaji bora ulimwenguni, amejigamba Cristiano Ronaldo. Mreno huyo mwenye miaka 30 ambaye ni mshindi mara tatu wa mchezaji bora wa dunia na mfungaji bora wa Real Madrid ameiambia BBC.

Sihititaji kusma, niko katika historia ya mpira, mimi ni legend. Namba zinasema kila kitu. Ronaldo ambaye alijiunga Real akitokea Manchester United mwaka 2009 kwa kitita cha Pauni milioni 80 amesema amefikia kiwango kiwango cha kushangaza kwa kipindi cha miaka 8 iliyopita na anataka kuendelea kucheza kwa misimu mingine mitano au sita.

Rekodi yake inaonyesha ana magoli 504 katika mechi 760. "Mawazoni mwangu mara zote mimi ndiye bora. Sijali watu wanachofikiria, wanachosema. Mawazoni mwangu, siyo mwaka huu pekee lakini mara zote mimi ni bora" Ronaldo aliendelea kujigamba.

Ronaldo alikuwa ameulizwa anajilinganishaje na mshambuliaji wa Barcelona na Algentina Lionel Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia mara nne akiwa na goli 418 za mechi 492 alizochezea klabu. "Ni maoni, ninaheshimu maoni. Labda kwa mawazo yako unaona Messi ni bora kuliko mimi lakini akilini mawazoni mwangu mimi ni bora kuliko yeye. Ni rahisi"

Ronaldo alijiunga Manchester United akitokea Sporting Lisbon mwaka 2003 kwa pauni milioni 12.2 akafunga magoli 118 katika mechi 292. Tangu ameahamia Madrid ambako yupo kwa makataba mpaka 2018 amefunga magoli 326 katika mechi 314.

Kuhusu iwapo kuna siku atarudi kuichezea Manchester United, Ronaldo amesema, hakuna aijuaye kesho lakini hapa alipo Madrid ana furaha tele japo kwanza anasikitika kuona ilipo hivi sasa kwa kuwa angependa iwe Machester ya kipindi kile cha miaka saba iliyopita.

Ronaldo pia amemuongelea Mourinho akasema, sishangazwi kwa sababu katika soka chochote kinaweza kutokea. Nilifanya naye kazi kwa miaka miwili naujua uwezo wake. Najua siyo yeye tu lakini pia Chelse iko katika wakati mgumu. Mimi ni Mreno ninataka kumwona mreno akiwa juu. Namtakia aondokane na wakati huu mgumu na awape furaha mashabiki wa Chelsea.