S Leone yatarajia kutangazwa haina Ebola

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Densi ya kumalizwa kwa ebola Sierra Leone

Kumekuwa na sherehe za kufana nchini Sierra Leone wakati raia wanaposubiri tangazo rasmi la shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa taifa hilo sasa halina maradhi ya Ebola.

Mlipuko huo uliwaua zaidi ya watu 4,000 kwa muda wa miezi 18 iliyopita.

Maelfu ya watu walijitokeza katika barabara za mji mkuu wa Free Town usiku wa manane, wakiadhimisha siku 42 tangu tukio lo lote la maradhi hayo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Sierra Leone wafurahia kumaliza ebola

Wengi walikusanyika karibu na mti mkubwa wa pamba katikati mwa jiji, wengine wakiwasha mishumaa kuwakumbuka waliofariki kutokana na maradhi hayo.

Walicheza densi za furaha wakati wote.