Misa ya wahanga wa ajali ya ndege ya Urusi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Misa ya wahanga wa ajali ya ndege ya Urusi

Ibada ya kuwakumbuka watu waliofariki katika ajali mbaya ya ndege ya Urusi katika rasi ya Sinai nchini ya Misri juma lililopita, inaendelea katika mji wa St Petersburg.

Maombi katika kanisa la mtakatifu Isaac yatafanyika sambamba na kupigwa kwa kengele mara 224, kwa heshima ya watu 224 waliofariki, ambao wengi wao walikuwa raia wa Urusi.

Maafisa wakuu jijini Moscow wanasema kwamba, bado wanatafuta chaanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.

Image caption Lakini tayari wamesema kuwa huenda ikawa ni bomu lililosababisha ajali hiyo.

Lakini tayari wamesema kuwa huenda ikawa ni bomu lililosababisha ajali hiyo.

Kiongozi mkuu wa kundi la wachunguzi, Ayman el Mokadem, amesema kuwa, kikosi chake bado hakijabaini aina ya sauti hiyo au kilichosababisha ajali hiyo.

Amethibitisha kuwa yamkini ndege hiyo ilipasuka msamba ikiwa bado angani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maombi katika kanisa la mtakatifu Isaac yatafanyika sambamba na kupigwa kwa kengele mara 224

Aidha inadaiwa kuwa data za ndege zinaonyesha kuwa gia ya ndege ilikuwa bado mahali pake hadi ilipoanguka - hii ikiashiria kuwa marubani walikuwa hawajapata tahadhari yoyote kwamba kulikuwa na matatizo yoyote ya injini.

Wakati huohuo Uingereza imetuma ndege tano Misri kuwaondosha raia wake nchini humo.

Taarifa zake za kijasusi zilidai kuwa ndege hiyo ya urusi ilidunguliwa na bomu, lakini kiongozi mkuu wa uchunguzi huko Misri anasema kwamba uchunguzi unaendelea.

Utawala wa Urusi unasema kuwa itawachukua majuma kadhaa kuwaresha nyumbani zaidi ya watalii wake 8,000 kutoka mji wa utalii nchini Misri.