Buhari amfuta kazi mkuu wa kupiga vita rushwa

Haki miliki ya picha Buhari Twitter
Image caption Rais wa Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amemfuta kazi mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini humo.

Hata hivyo bado hajaeleza sababu zilizomfanya kumpiga kalamu Ibrahim Lamorde ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu 2011.

Rais Buhari alishinda kiti cha Urais nchini humo, katika uchaguzi uliofanyika mwaka huu.

Baraza lake la mawaziri linatarajiwa kuapishwa baadaye wiki hii, zaidi ya miezi mitano baada ya kuingia madarakani.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema Rais Buhari anataka kuhakikisha kwamba mawaziri wapya atakao wateua hawatatumia ofisi kwa faida zao binafsi.