Ukame mkali wanyemelea Ethiopia

Image caption Ethiopia

Umoja wa Mataifa umesema juhudi kubwa za msaada kimataifa zinahitajika nchini Ethiopia kuzuia janga la kibinadamu.

Umoja huo umesema uhaba wa chakula unaosababishwa na ukame unasambaa kwa haraka, na mwanzoni mwa mwaka ujao watu milioni 15 wanahitaji msaada wa chakula.

Uhaba wa mvua umepunguza mazao shambani kwa asilimia 90 katika maeneo yaliyoathiriwa vibaya na ukame huo.

Serikali ya Ethiopia imetenga kiasi cha dola za Marekani mia moja na milioni 90 kwa ajili ya dharura, hata hiyo Umoja wa Mataifa unasema juhudi zaidi zinahitajika.