Mkuu wa maabara ya kupima wanariadha ajiuzulu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Dawa za kusisimua misuli

Kiongozi mkuu wa maabara inayohusika na uchunguzi wa wanariadha wanaotumia dawa za kusisimua misuli nchini Urusi amejiuzulu.

Grigoriy Rodchenkov, amefanya hivyo siku moja tu baada ya wakala wa kuzuia matumizi ya dawa hizo kutoa taarifa yake inayoishutumu Urusi kuongoza katika udanganyifu wa wanariadha wake kutumia dawa za kusisimua misuli.

Waziri wa michezo wa Urusi amesema Bwana Rodchenkov ameamua kujiuzulu ili kuondokana tuhuma zote zilizopo.

Akizungumza na BBC, mkuu wa shirikisho la wanariadha nchini Urusi, Mikhail Butov amekiri kuwepo kwa tatizo.

Hata hivyo, amesema ni tatizo la kimtazamo katika kiwango cha ufundishaji.